CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA NA MIKOPO K.K.K.T. ARUSHA ROAD DYK
K.K.K.T. Arusha Road SACCOS Limited ni Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo.Ofisi yake ipo Plot No. 6, Bk 29 Area ‘‘C’’ karibu na Kanisa la K.K.K.T. Usharika wa Arusha Road Dodoma. Chama kilianzishwa Februari 2004 na kupata usajili nambari DOR 619 tarehe 25 Mei 2004. Pia Chama kina leseni (Licenced SACCOS)
Huduma zitolewazo na chama
- Kupokea Hisa, Akiba na Amana.
- Kutoa Mikopo yenye masharti nafuu
- Kutoa Elimu ya Ushirika na Ujasiriamal
Akiba na Amana
Chama kitatoa riba isiyozidi asilimia 5 kuanzia kima cha chini cha Akiba na 3 kwenye Amana alizonazo Mwanachama kuanzia kima cha chini cha shs. 100,000/=.
MADHUMUNI YA CHAMA
Madhumuni
- Kuinua na kuimarisha hali ya kiuchumi kwa Wanachama wake.
- Kupokea Hisa, Akiba na Amana kutoka kwa Wanachama na kuzitunza.
- Kutoa Mikopo yenye masharti nafuu kwa Wanachama wake.
- Kujenga tabia ya Wanachama ya kujiwekea akiba pamoja na kubuni na kuendesha miradi ya maendeleo ili kujiongezea kipato.
DIRA NA MWELEKEO WA SACCOSS
DIRA
K.K.K.T. ARUSHA ROAD SACCOS LTD inadhamiria kuwa SACCOS bora kanda ya Kati inayojitegemea kwa mtaji wa ndani, kuboresha maisha ya Wanachama wake kwa kuhimiza uwekaji wa Akiba na kutoa Mikopo kwa wakati ifikapo 2024.
MWELEKEO
K.K.K.T. ARUSHA ROAD SACCOS LTD itatoa huduma na bidhaa bora kwa Wanachama wake kwa kutumia fursa zilizopo katika kuwekeza na kujenga uwezo kiuchumi, kijamii na kibiashara kwa kuzingatia:-
- Uadilifu
- Usawa wa jinsia.
- Uwazi na ukweli.
- Upendo.
- Uwajibikaji na Demokrasia ya kweli.
UONGOZI NA USIMAMIZI
UONGOZI
KKKT ARUSHA ROAD SACCOS LTD inaongozwa na bodi yenye wajumbe 7 ambao wamechaguliwa katika mkutano mkuu wa uchaguzi wa tarehe 05/12/2020
Kazi na Wajibu wa Bodi:-
- Kusimamia shughuli zote za uchumi za Chama na kuhakikisha kuwa zinaendeshwa ipasavyo.
- Kutekeleza kikamilifu maazimio na maelekezo ya Mikutano Mikuu.
- Kufanya maamuzi kuhusu udahili wa wanachama wapya, kujiuzulu wanachama, kusimamishwa uanachama na kusimamishwa kwa wajumbe wa Bodi na kuwasilisha masuala hayo kwenye Mkutano Mkuu kwa ajili ya kujadiliwa na kutolewa maamuzi ya mwisho
- Kuchukua Uamuzi ikingojea uthibitisho wa Mikutano Mikuu, juu ya kupokelewa Wanachama wapya, kujiuzulu Wanachama, kusimamishwa kwa Wajumbe wa Bodi.
- Kubuni na kutayarisha Sera na Kanuni za uendeshaji Chama zinazohusu Fedha, Biashara, Utawala, Mikopo, Bohari n.k. ili kufanikisha madhumuni ya Chama.
- Kuwasilisha kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama Taarifa ya Hali ya Uchumi na Maendeleo ya Chama pamoja na Hesabu ya Mapato na Matumizi, Mizania iliyothibitishwa kwa mwaka uliopita na Makisio ya Mapato na Matumizi ya mwaka unaofuata.
- Kupokea na Kujadili taarifa za Kamati ya Mikopo na Kamati ya Usimamizi.
- Kuteua Mwanachama atakayeshika nafasi iliyoachwa wazi kwenye Bodi. Aliyeteuliwa atashika nafasi hiyo mpaka Mkutano Mkuu mwingine unaofuata ambapo nafasi iliyoachwa wazi itajazwa kwa kupigiwa kura au kwa uthibitisho.
- Kumwezesha mtu aliyeidhinishwa kukagua vitabu vya Chama na kuhakikisha kuwa hatua zinachukuliwa kutokana na Taarifa ya Ukaguzi.
- Kuhakikisha kuwa Wanachama wanafuata na kuzingatia Masharti haya, Taratibu na Mikataba mbalimbali.
- Kufungua akaunti Benki na kuhakikisha kuwa fedha zote za Chama zinatunzwa katika Benki.
- kuandaa mpango mkakati, mpango wa biashara na programu ya utekelezaji wake.
- Kuhakikisha kwamba Chama kinawakilishwa katika mashtaka yote.
- Kuhakikisha kuwa mali, bidhaa, vifaa, na nyaraka / hati za Chama zinahifadhiwa vizuri na kwa usalama.
- Kuteua Wajumbe watakaotia saini kwenye hundi za Chama.
- Kuajiri na kuteua watumishi wenye sifa za kutosha kutenda shughuli za Chama wakiwemo Meneja / Katibu, Mhasibu / Mweka Hazina, au watumishi wengine kutokana ama miongoni mwa Wanachama au nje ya Wanachama ambao wataendesha shughuli za kila siku za Chama.
- kuingia mikataba mbalimbali kwa niaba ya chama.
- kuingia mikataba mbalimbali kwa niaba ya chama.
- Kupendekeza kwenye Mkutano Mkuu mabadiliko au viwango vya riba au masharti ya ulipaji mikopo na / au mgawanyo wa mikopo (amortization).
- Kuandaa marekebisho ya Masharti ya Chama pale itakapobidi na kuwasilisha kwenye Mkutano Mkuu.
- Kutayarisha / kuchapisha Hati za kumiliki Hisa kwa ajili ya Wanachama.
Wajumbe wa bodi kwa kipindi cha 2020-2023
# |
Jina |
Nafasi Katika Bodi |
1 |
Mr Emmanuel B. Ulomi |
Mwenyekiti |
2 |
Mrs Stella Mwanga |
Makamu Mwenyekiti |
3 |
Rev. Mary C. Madelemo |
Mjumbe |
4 |
Dr Emmanuel Ayo |
Mjumbe |
5 |
Dr Anastasia R. Njiku |
Mjumbe |
6 |
Dr Christina G. Mandara |
Mjumbe |
7 |
Mrs Magreth Matowo |
Mjumbe |
USIMAMIZI
KKKT ARUSHA ROAD SACCOS LTD inasimamiwa na kamati ya usimamizi ambayo inaundwa na wajumbe watatu (3) ambao wamechaguliwa katika mkutano mkuu wa uchaguzi wa tarehe 05/12/2020
Kazi na Majukumu ya Kamati ya Usimamizi
Kamati ya Usimamizi itafanya kazi na kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Ushirika, 2013, Kanuni zake kama ifuatavyo:-
- kufanya mapitio ya mara kwa mara kuhusu usahihi wa kumbukumbu za hesabu.
- kutoa taarifa kwenye kila kikao cha kawaida cha Bodi.
- kutoa mapendekezo ya kuboresha Sera, taratibu za uendeshaji na udhibiti wa ndani na kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wake.
- kuandaa taarifa ya ukaguzi na usimamizi wa hesabu ya mwaka na kuiwasilisha kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka kama Mkaguzi wa nje hataweza kufanya hivyo
- kupendekeza kwa Bodi wakaguzi wa nje watakaofanya ukaguzi kwa mwaka wa fedha unaofuata endapo sio COASCO
- kutekeleza majukumu mengine kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Ushirika na sheria nyingine pamoja na kanuni zake.
- Kusimamia fedha na mali zote za Chama kwa niaba ya Wanachama.
- Kuamuru kufanyika angalau mara moja katika miezi mitatu (3) uchunguzi wa shughuli za Chama, pamoja na ukaguzi wa vitabu na itatengeneza au itaamuru utengenezaji wa taarifa itakayotolewa kwa Bodi kwa maandishi na itakagua au itaamuru ukaguzi wa mwaka ufanyike na taarifa yake itolewe kwa maandishi katika Mkutano Mkuu wa Mwaka ufuatao.
- Kufuatilia maendeleo ya miradi mikubwa ya Wanachama ambayo imepatiwa mikopo na Chama mpaka wahusika wanapomaliza marejesho.
- Kutayarisha taarifa ya maandishi juu ya hali ya fedha na huduma zitolewazo kwa Wanachama kwa Bodi na Mkutano Mkuu na nakala kwa Afisa Ushirika wa Wilaya na Mkoa, kila baada ya miezi mitatu (3) ya Mwaka wa Fedha wa Chama.
- Kutafuta ufumbuzi wa udhaifu wa Uongozi na kushauri Mkutano Mkuu ipasavyo.
Wajumbe wa Kamati ya Usimamizi
# |
Jina |
Nafasi Katika Bodi |
1 |
Mrs Ndeningwa Urassa |
Mwenyekiti |
2 |
Mr Emanuel Matowo |
Katibu |
3 |
Ms Pendo E. Senguruka |
Mjumbe |
Watendaji
KKKT Arusha Road Saccos ina jumla ya watendaji (13) ambao ni:
# |
Jina |
Nafasi Katika Bodi |
1 |
Mr Andrew P. Ntomola |
Meneja |
2 |
Mr Daudi D Lazaro |
Mhasibu |
3 |
Mr Gabriel Challo |
Afisa Mikopo |
4 |
Mr Prosper I Munuo |
Afisa Mikopo msaidizi |
5 |
Ms. Devota P Mosha |
Karani |
6 |
Ms. Tuli Z Lukandala |
Karani |
7 |
Ms. Naomi J Ghula |
Karani |
8 |
Mr. Peter Isangya |
Mkaguzi wa ndani |
9 |
Mr Shambiti S. Shilinde |
Mlinzi |
10 |
Mr Japhet M. Nyangembe |
Mlinzi |
11 |
Mr Joram M Msaghaa |
Mlinzi |
12 |
Mr Ezekiel M. Mazengo |
Mlinzi |
13 |
Ms. Veronica H. Massawe |
Mhudumu |
MUUNDO WA UONGOZI K.K.K.T. Arusha Road SACCOS
MUUNDO WA UONGOZI:
Muundo wa Uongozi unaojumuisha ngazi za maamuzi kwa mujibu wa Sheria ya Ushirika Nambari 6 ya mwaka 2013 ni kama unavyoonyeshwa katika mchoro Na. 1 unaofuata:-
BODI YA USIMAMIZI
Alphonce John
Rohit Gregory
Alex Brandson
Amelia Axson
Stephan George
SHERIA NA KANUNI
Sheria, Kanuni & Miongozo
Sheria za kiserikali
Mikopo ya Maendeleo
A) MIKOPO YA BIASHARA
Mikopo ya aina hii itatolewa kwa Wanachama binafsi na Wanachama katika vikundi na taasisi, kwa ajili ya kuendeleza biashara, siyo kwa ajili ya kuanzishia biashara mpya ambayo mkopaji hana uzoefu nayo. Kwa sababu kwa biashara mpya kuna uwezekano mkubwa wa kushindwa kurejesha mkopo, kwani mkopaji anahitaji muda wa kuelewa uendeshaji wa biashara yake mpya. Mikopo ya aina hii ni kwa ajili ya biashara za aina zote, isipokuwa Ufugaji, kama ifuatavyo:-
- Biashara za bidhaa kama Duka, Migahawa, Mazao ya Kilimo na Mifugo, Grocery, n.k.
- Biashara za Huduma kama Usafirishaji, Huduma za Mawasiliano, Matibabu, Ushauri Kifani, n.k.
- Biashara za Uzalishaji bidhaa kama Viwanda vidogo na vya kati, Ufundi wa aina zote, n.k.
- Biashara ya fedha kama Duka la kubadilisha Fedha lakini kamwe isiwe biashara ya kukopesha fedha.
Masharti mengine:-
- Mikopo hii itatolewa baada ya Afisa Mikopo kufanya tathmini ya kushtukiza ya biashara ya mwombaji na kuridhika nayo kwa kulinganisha na kiasi cha mkopo unaoombwa na muda wa marejesho ili kupima uwezo wa mkopaji kulipa mkopo.
- Tathmini ya Afisa Mikopo ndiyo kigezo cha kiasi cha mkopo na muda wa marejesho. Hivyo Kamati itakuwa na uwezo wa kupunguza au kuongeza kiasi na muda wa mkopo.
- Marejesho ya mikopo yatafanyika hata kama biashara imefilisika au imepatwa na janga la aina yoyote.
- Janga la Biashara halitamwondolea mkopaji wajibu au jukumu la kulipa deni, lakini linapotokea janga, mkopaji anatakiwa atoe maelezo ya maandishi juu ya janga lililotokea. Maelezo hayo yatapelekwa kwa Meneja yakiambatana na ushahidi wa kisheria. Hili linafanyika ili Bodi iweze kuelewa yanayomsibu Mwanachama na kuweza kutumia busara kumshauri na kuchukua hatua zinazostahili.
- Biashara lazima iwe HALALI KISHERIA.
B) MIKOPO YA UFUGAJI
Mikopo ya aina hii itatolewa kwa waombaji kwa ajili ya shughuli za ufugaji kwa lengo la biashara siyo chakula cha familia. Aina ya mifugo itakayofugwa na mwombaji mkopo ni ile inayoendana na hali ya hewa na mazingira ya Dodoma kama ifuatavyo:-
- Wanyama:- ng’ombe wa nyama, mbuzi, ng’ombe wa maziwa, nguruwe, sungura, kondoo n.k.
- Kuku:- Kuku wa Nyama, kuku wa mayai, kutotolesha vifaranga, n.k.
Shughuli za ufugaji zitakazopewa mkopo ni zifuatazo:-
- Ununuzi wa mifugo yenyewe.
- Ujenzi wa miundo mbinu na vifaa vya shughuli za ufugaji.
- Madawa na vyakula.
- Malipo ya ushauri na utaalam.
- Usafirishaji na nauli.
Masharti mengine:-
- Mikopo kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu itatolewa kwa mkupuo mmoja.
- Mwombaji atatakiwa airidhishe Kamati ya Mikopo kuwa ataweza kurejesha mkopo na riba hata kama mifugo itakumbwa na majanga yoyote.
- Mwombaji atakayekutwa na majanga, atatakiwa alete maelezo ya maandishi kwa Meneja akieleza janga lililomsibu.
- Mkopaji atalazimika kufuata ufugaji wa kisasa na kitaalam. Kamati ya Mikopo itabuni utaratibu wa kuthibitisha juu ya hili.
- Kamati ya Mikopo itafanya ufuatiliaji na tathmini kwa kutembelea na kuambatana na wataalam wa mifugo wakati wowote watakapoona ni muhimu kufanya hivyo.
- Ufugaji utakaopewa mkopo ni ule unaofanyika ndani ya Mkoa wa Dodoma tu.
- Mkopaji anatakiwa awe na uzoefu wa ufugaji siyo chini ya miaka mitatu (3).
- Kamati ya Mikopo itapaswa ijiridhishe kuwa ufugaji utakaofanywa na mwombaji wa mkopo unafuata na unakidhi masharti ya Sheria ya Nchi, Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
C) MIKOPO YA ELIMU
Mikopo ya aina hii itatolewa kwa Wanachama kwa ajili ya kugharimia gharama za Elimu kwa Mwanachama binafsi, ndani ya kikundi/taasisi au mtoto/ndugu wa Mwanachama. Mikopo itatolewa kwa ajili ya aina zote za gharama za Elimu bila kujali Elimu hiyo inapatikana wapi.
Masharti mengine:-
- Mwombaji atatakiwa kutaja gharama ya Elimu kwa mwaka mzima.
- Katika gharama za Elimu za mwaka mzima, mwombaji atawajibika kueleza ni kiasi gani anahitaji kitokane na fedha za mkopo.
- Kwa kuwa mkopo wa Elimu hauzalishi kipato cha kumwezesha kurejesha mkopo na riba, hivyo mwombaji atawajibika kueleza ni kwa njia gani atarejesha mkopo huo.
D) MIKOPO YA UJENZI
Mikopo ya aina hii itatolewa kwa ajili ya shughuli zozote zinazohusu ujenzi wa nyumba ya kuishi au ya biashara pindi itakapokuwa imekamilika.
Masharti mengine:-
- Mwombaji atawajibika kueleza ni hatua gani ya ujenzi anayoombea mkopo. Hatua ni kuanzia ujenzi wa msingi hadi umaliziaji.
- Mwombaji itabidi airidhishe Kamati ya Mikopo ni kwa njia gani ataweza kurejesha mkopo na riba kwani wakati wa ujenzi hakuna uzalishaji wa kipato.
- Mwombaji ni LAZIMA katika maombi yake aambatanishe na kivuli cha hati ya kumiliki kiwanja na ramani iliyopitishwa na mamlaka husika, ili kuepuka migogoro ya umiliki.
-
Mkopo na Riba utarejeshwa kwa mujibu wa mkataba hata kama ujenzi umekwamishwa kwa njia yoyote ile ikiwemo:-
- Kuzuiwa na mamlaka ya uendelezaji mji.
- Kupatwa na janga lolote lile.
D) MIKOPO YA VIWANJA
Aina hii ya Mikopo itatolewa kwa Mwanachama mwenye hitaji la kupata kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa jengo lakini kwa wakati husika hana uwezo wa kifedha kulipia gharama za ununuzi kwa mkupuo mmoja. Hivyo Chama kitagharamia kununua viwanja toka Mamlaka husika na kuwakopesha Wanachama wake kwa utaratibu wa Mikopo ya Biashara.
Mikopo ya Dharura
A) MIKOPO YA DHARURA JAMII
Mikopo ya aina hii itatolewa kwa Mwanachama kwa lengo la kumsaidia Mwanachama aliyekabiliwa na matukio ambayo hayakutarajiwa kutokea kwa namna yoyote, na kutokea kwake yamethibitika. Mfano:-
- Kuuguliwa na Ndugu, Mtoto, Mzazi.
- Kuugua kwa Mwanachama mwenyewe.
- Janga la moto, kimbunga, mafuriko, matetemeko.
- Kuibiwa.
- Sherehe, Misiba n.k
Utoaji wa Mikopo ya dharura Jamii:-
Mikopo ya aina hii itatolewa kwa kuzingatia yafuatayo:-
- Kiwango cha juu cha mkopo kwa mara moja kitakuwa siyo zaidi ya nusu (1/2) ya akiba za Mwanachama. Hata hivyo kiwango cha juu cha mkopo wa Dharura Jamii hakitazidi Tsh. 2,000,000/= (Milioni mbili).
- Idhini ya kutoa mkopo ni Mjumbe wa Zamu na Meneja/Afisa Mikopo/Mhasibu
- Mkopo utatolewa si zaidi ya saa 24 tangu kuletwa kwa ombi.
- Mkopo huu utatolewa hata kama Mwanachama ana mkopo mwingine wa kawaida anaoendelea kurejesha.
- Pamoja na kipengele kidogo cha juu cha (d), mkopo hautatolewa kwa wakopaji walioshindwa au waliochelewesha rejesho hata moja tu la mkopo aliyonao Chamani.
- Muda wa kurejesha Mikopo ya aina hii ni miezi minne (4) tangu tarehe ya kutolewa kwa mkopo.
Masharti mengine:-
- Dhamana ya Mikopo ya dharura ni Akiba na Amana za mkopaji Chamani, hivyo haitahitajika dhamana ya Wanachama wawili (2).
- Mkopo wa dharura hautatolewa endapo Mwanachama bado anadaiwa mkopo mwingine wa dharura.
- Mwanachama aliyebakiza rejesho moja la mkopo wa dharura anaweza kuomba na kupewa mkopo mwingine wa dharura baada ya kulipa rejesho lililobakia.
- Kwa Mwanachama mwenye mkopo wa kawaida anaoendelea kuulipa, atatakiwa kuthibitisha uwezo wake wa kurejesha Mikopo yote miwili ( wa kawaida na wa dharura) na riba zake. Watakaoidhinisha wajiridhishe kwa uwezo huo wa mwombaji.
- Kutakuwepo na Mkataba maalum.
B) MIKOPO YA DHARURA YA BIASHARA NA KUJIKIMU
- Mikopo ya aina hii itatolewa kwa Wanachama wafanyabiashara wanaohitaji fedha kwa dharura stahiki ya kibiashara, na Wanachama wanaohitaji fedha za kujikimu.
- Kiasi cha juu kukopeshwa Mwanachama kitazingatia mwenendo wake wa urejeshaji na uaminifu. Hata hivyo kiwango cha juu hakitazidi nusu (½) ya kiasi cha Akiba za mkopaji.
- Viwango vya riba kwa aina hii ya Mikopo itakuwa ni asilimia tatu (3%) kwa mwezi.
-
Mikopo ya aina hii itapitishwa na kuidhinishwa na:-
- Mjumbe wa Zamu
- Meneja
- Afisa Mikopo
- Mhasibu
-
Utaratibu wa kupata aina hii ya Mikopo utakuwa kama ifuatavyo:-
- Mkopaji awe na dhamana ya gari, hati ya nyumba n.k
- Mkopaji anatakiwa kuandika mchanganuo kwa kifupi kuhusiana na Biashara husika anayoombea mkopo wa Dharura ya Biashara
- Atalipia fomu na mkataba wa mkopo shs. 20,000/=
- Muda wa kurejesha hautazidi miezi sita (6).
- Kwa aina hii ya Mikopo, adhabu kwa mkopaji atakayechelewesha marejesho itakuwa asilimia tano (5%) ya kiasi kilichocheleweshwa kila mwezi.
- Afisa Mikopo atatembelea Biashara au Shughuli ya Mkopaji kwa lengo la kujiridhisha na uhitaji wa Dharura hiyo.
C) MIKOPO YA CHAPCHAP
Aina hii ya mkopo itatolewa kwa Mwanachama mwenye uhitaji wa mkopo wa haraka kwa ajili ya kutatua shida ndogondogo zilizojitokeza. Kiwango cha mkopo hakitazidi tshs 200,000. Muda wa kurejesha hautazidi mwezi mmoja. Riba ya mkopo huu ni asilimia 10 kwa mwezi.
Taratibu za Utoaji Mikopo
- Mikopo inatolewa hadi mara tatu (3) ya Akiba ya Mwanachama.
- Kiwango cha juu cha mkopo ni shs. 50,000,000/=
- Riba ya mkopo ni asilimia 2.2 kwa mwezi njia ya kupungua usawa (reducing balance).
- Muda wa marejesho ni kati ya mwezi 1 hadi miezi 24, kulingana na ukubwa wa mkopo.
- Adhabu ya asilimia 3 ya kiasi cha mkopo kilicho cheleweshwa itatozwa kwa mwezi.
- Mkopaji aweke dhamana inayolingana na thamani ya mkopo au zaidi.
- Mkopaji awe na wadhamini wasiopungua wawili ambao ni Wanachama.
UANACHAMA
MWANACHAMA WA ARUSHA ROAD SACCOS
Mtu yeyote anaweza kuwa mwanachama wa Arusha road akiwa na sifa zifuatazo:-
- Awe Mkazi wa Manispaa ya Dodoma, mwenye umri usiopungua miaka kumi na nane (18).
- Awe na akili timamu na tabia njema
- Awe anafanya kazi/shughuli yoyote halali na kuishi katika eneo la Chama na anayekubali kufuata Masharti haya.
- Awe tayari kushiriki kikamilifu katika shughuli zote za Chama.
- Asiwe na shughuli binafsi zinazofanana na shughuli za Chama.
- Awe amelipa kiingilio, hisa za uanachama na kuweka akiba kwa kiwango kilichowekwa kwa mujibu wa masharti haya na awe tayari kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za chama.
HAKI ZA MWANACHAMA
Mwanachama yeyote wa Arusha road saccos ana haki zifuatazo:-
- Kushiriki kikamilifu katika shughuli za Chama na kuhudhuria Mikutano yote inayomhusu.
- Kushiriki katika kutoa Uamuzi wa mambo mbalimbali katika Mikutano Mikuu.
- Kupiga kura chini ya misingi ya mtu mmoja kura moja bila kujali idadi ya hisa anazomiliki.
- Kuchagua na/au kuchaguliwa katika Uongozi wa Chama.
- Kuwa na haki sawa kuhusu mali ya Chama na kudhibiti ipasavyo matumizi yake.
- Kupatiwa huduma zozote zinazotolewa na Chama.
- Kupatiwa Masharti, Mizania, Mihutasari ya Mikutano na nyaraka nyingine za Chama.
- Kuitisha Mikutano ya Wanachama kwa mujibu wa Kanuni na Masharti haya.
- Kupatiwa mkopo kulingana na Masharti na Sera ya Akiba na Mikopo ya Chama.
- Kupewa kitabu cha Akiba (passbook).
WAJIBU WA MWANACHAMA
Mwanachama yeyote wa Arusha road saccos ana wajibu wa :-
- Kulipa Kiingilio na Hisa na kuweka Akiba na michango yote iliyoamuliwa na Mkutano Mkuu.
- Kufuata Sheria ya Vyama vya Ushirika na Kanuni zake, Masharti ya Chama, Sera za Chama na Maamuzi ya Mikutano Mikuu.
- Kurejesha mkopo kwa wakati uliopangwa kama Sera ya Utoaji, Ufuatiliaji na Ufutaji wa Mikopo inavyoelekeza.
- Kutoa michango mbalimbali katika kuendeleza madhumuni ya Chama.
- Kubeba dhamana endapo janga lolote litatokea kwa Chama au Wanachama.
- Kuwa mwaminifu na kuonyesha ushirikiano katika kutekeleza shughuli za Chama.
- Kumdhamini mkopo Mwanachama mwenzake. ( Mwanachama aliyedhamini hatakuwa Na haki ya kudhaminiwa Na Mwanachama aliyemdhamini katika kipindi kilekile Kama Sera ya Utoaji, Ufuatiliaji na Ufutaji wa Mikopo inavyoelekeza ).
- Kulipa mkopo alioudhamini endapo mdhaminiwa / mkopaji atashindwa kulipa mkopo wake.
- Kuwashawishi wasio Wanachama waweze kujiunga na Chama.
- Kuhudhuria Semina na Mafunzo yanayotolewa na Chama.
- Kuhudhuria Mikutano yote inayomhusu kwa wakati uliopangwa.
- Kulinda na kudhibiti mali za Chama zisitumike visivyo.
- Kulinda na kutetea hadhi na sifa ya Chama.
- Kuteua Mrithi.
- Kudhamini Chama.
JINSI YA KUJIUNGA
Arusha Road Saccos ina taratibu mbili za kujiunga ambazo ni:-
- Utararibu wa kawaida
- Utaratibu wa wa promosheni
- UTARATIBU WA KAWAIDA
- Mtu anaweza kujiunga na chama kwa kufuata utaratibu na sheria za kawaida zilizo ainishwa na chama.
- UTARIBU WA PROMOSHENI
- Utaratibu wa promosheni unaambatana na vitu vifuatavyo:-
-
- Kiingilio ni shs. 20,000/=
- Fomu ya Uachama shs 10,000/=
- Akiba ya kuanzia isiyopungua shs 100,000/=
- Hisa mbili (2) zenye thamani ya shs. 20,000/= ikiwa hisa moja ni shs. 10,000/=
- Mwanachama atatakiwa kuongeza Hisa zake kufikia idadi ya Hisa mia moja kwa kipindi cha miezi 12
- Picha tatu (3) za “Passport size” zilizopigwa hivi karibuni
- Kitambulisho cha Taifa
- Mwanachama wa kumtambulisha
SIKU ZA KAZI
Siku |
Muda |
Jumatatu – Ijumaa: |
saa 3:00 asubuhi hadi saa 11:00 jioni |
Jumamosi: |
saa 3:00 asubuhi hadi saa 7:00 mchana |
Matukio & Matangazo
BIDHAA NA HUDUMA ZITOLEWAZO NA K.K.K.T. Arusha Road SACCOS
BIDHAA
- Kupokea Hisa
- Kupokea Akiba
- Kupokea Amana
- Kutoa Mikopo
HUDUMA
- Uwakala wa CRDB Fahari
- Uwakala wa MPESA
- Uwakala wa Bima (BUMACO)
HISTORIA YA CHAMA
K.K.K.T. ARUSHA ROAD SACCOS LTD ilianzishwa mwezi Februari 2004. Chama kilisajiliwa mwezi Mei 2004 na kupata nambari ya usajili DOR 619. Ofisi ya Chama ilikuwa kwenye jengo la Kanisa la K.K.K.T. Usharika wa ARUSHA ROAD, AREA “C” Dodoma. Mwishoni mwa mwezi Mei 2011, chama kilifanikiwa kuahamia katika jengo lake lililopo karibu na Kanisa hilo, kwenye kiwanja Plot 6 Block 29 Area “C”.
MAWASILIANO
Anuani
Area C, Kiwanja cha Ndege,
Plot No 6, Block 29
Dodoma Mjini, Dodoma.
Wasiliana nasi
(+255) 26351590
info@saccoss.co.tz